UONGOZI wa Yanga umesema kuwa timu nyingi ambazo wanakutana nazo zinawakamia jambo linaloongeza ugumu wako kupata matokeo.
Ofisa uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa timu nyingi zinatambua kwamba Yanga ni timu kubwa hivyo wakiifunga kwao itawaongezea hali ya kujiamini.
"Unajua timu nyingi zinapocheza na Yanga zinatambua kwamba zinacheza na timu kubwa, zinakamia mwanzo mwisho zikiwa na malengo ya kupata hali ya kujiamini hilo pia linachangia timu kushindwa kupata matokeo.
"Lakini hakuna ambacho kinashindikana bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na kurejea kwenye ubora wetu mashabiki watupe sapoti,".
Yanga kesho itakuwa Uwanja wa Taifa kumenyana na Gwambina mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya nne mbele ya Coastal Union ya Tanga, Mkwakwani baada ya kutoka kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Tanzania, Ushirika, Moshi.
Kwenye ligi ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 41 imecheza mechi 22.

hiyo mbona rahisi..ni kiasi cha kuziambia timu zinazobana ziachie. kama Yanga wanajua Simba wanabebwa au wanamtumia Mo..Basi nao Yanga wafanye hivyo..Bil 1.8, wachezaji 20 wapya katika msimu mmoja...Mtaalamu toka Binafica-Ureno..Hivi nini kweli kinawashinda Yanga.. Cha muhimu unapokuwa unashindwa tafuta sababu za msingi...acha nyimbo za wenzako wanapewa penalti, wanafunga kwa offside, wanapuliza dawa...Na takwimu hazifichi kama kuna timu amabayo inaongoza kwa kubebwa basi ni Yanga..Na jusi mechi ya polisi ilidhihirisha
ReplyDeleteYanga wanabebwa tu
ReplyDeleteIkiwa kukamiwa Simba kinara wa point na magoli inakamiwa Mara kumi kuliko wa Jangwani na mchezaji anaekamiwa kuliko wachezaji wote ni Kagere na la ajabu na la ajabu kuwa yeye Kagere ndie kinara wa mabao na Simba ndiyo ya juu kwa magoli na pointi 62 ambazo hazikaribiwi na yeyote kimyakimya bila ya makelele au kulalamika ovyoovyo. Tafuteni sababu nyengine
ReplyDeleteSIMBA WANAZO PESA NA WANATOA KWA WACHEZAJI WA KILA TIMU INAYOCHEZA NA YANGA NA NDIYO INAYOWAPA NGUVU YA KUKAMIA NA KUCHEZA KWA NGUVU ZOTE NA YANGA HIVI SASA HAWANA PESA KAMA HIZO - SASA ELEWA HAPO KAMA KWELI UNAELEWA FITNA ZA SOKA .
ReplyDeleteNA ZAHERA ALISHASEMA KUWA KUFANYA HIVYO SI DHAMBI NA HATA EUROPE WANAFANYA
Kwa hiyo na Yanga wanafanya hivyo ila wanatoa mshiko kidogo! Sasa povu la nini si watafute hela zaidi. Kama wanaweza kuleta uwanjani mashabiki wa kizungu watakosa hela ndogo kama hiyo? Timu kubwa imegeuka kuwa mourners.
DeleteMalalamiko fc,nyie ni vilaza namba moja katika vilaza bora kabisa basi nyinyi ndio vinara wa vilaza,na bado gwambina anakwenda kuwafanya mboga kesho,wakati mkiendelea kujiita mabingwa wa jadi,mabingwa wa kihistoria,timu ya wananchi,wenzenu wanajiita SIMBA SPORT CLUB na huku mkiendelea kuimarisha kikosi wenzenu wanakusanya alama zakujihakikishia ubingwa,endeleeni kuaminisha uma kwamba nyinyi ni mabingwa na simba wanabebwa ila hata CAF wanaujua mziki wa SIMBA SPORT CLUB na rank zimetoka juzi nadhan yanga amejiona alivyotupwa mkiani wakati simba akifukuzia 20 bora,acheni kudanganya uma yanga bado changa sana kwa simba,na lazima mjue kwamba ukubwa wa timu sio umri bali ni ubora wa kikosi na benchi la usimamiz ambavyo hupimwa kwa matokeo bora yanayopatikana kwenye kila ligi ambayo timu itakua ikishiriki.
ReplyDelete