UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo kwenye mchezo wao dhidi ya Stand United utafanya mabadiliko makubwa ya kikosi ili kuwapa nafasi wachezaji ambao walikuwa hawapati nafasi kucheza.
Simba itashuka Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga kumenyana na Stand United kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora.
Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema kuwa wanatambua kwamba wana mchezo mgumu ila watafanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi chao kitakachovaana na Stand United leo.
"Simba ina wachezaji wengi na hatuwezi kuwatumia wote 29 kwenye mechi moja ni lazima tuchague aina ya wachezaji ambao tunawahitaji, tutafanya mabadiliko kwenye kikosi kitakachocheza dhidi ya Stand United,".
hapo ndio mtapata kichapo kisha coach atafukuzwa kama kawaida yenu mikia
ReplyDeleteTunagawana brother mbona mnashindwa kuelewa mfumo wa uendeshaji wa ligi??sasa simba achukue makombe yote ili faida yyake kwa taifa itakua iko wapi kwenye kuitangaza nchi kisoka?lazima timu nyingine ichukue na sio simba eleweni mfumo na utaratibu,kumbuka liver amekula tano akala tena moja cjui mbili kwahyo ndivyo vilivyo acheni kukariri pasi kuelewa.
ReplyDelete