February 22, 2020


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa ana kazi ngumu leo mbele ya Azam FC iliyo chini ya Arstica Cioaba.

Namungo itaikaribisha Azam FC Uwanja wa Majaliwa, majira ya saa 10:00.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema wataingia kwa tahadhari kubwa kuzipata pointi tatu mbele ya Azam FC kwani mechi zao kubwa ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Simba imewapa nguvu ya kujiamini.

"Tunacheza na timu yenye uzoefu hivyo tunatakiwa kuingia kwa tahadhari na kupambana kuzitafuta pointi tatu.

"Tutakuwa uwanja wa nyumbani nasi tukijiamini baada ya kucheza mechi nyingi ngumu ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Simba hiyo itakuwa nguzo yetu kupata ushindi," amesema.

Namungo kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia pointi 40 na imecheza mechi 22.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic