February 22, 2020


MOHAMED Kijuso, Kocha Msaidizi wa Mbeya City amesema kuwa watapambana leo mbele ya Mtibwa Sugar ili kupata pointi tatu zitakazookoa jahazi la timu yake.

Mbeya City ipo nafasi ya 18 kwenye msimamo imejikusanyia pointi 21 baada ya kucheza mechi 23.

"Tupo kwenye hali mbaya kwa sasa kwenye ligi jambo linalotufanya tupambane kutafuta matokeo, kuna ushindani mkubwa nasi tunajipanga kurejea kwenye ubora wetu.

"Kitu kimoja pekee kitatubakiza kwenye mstari ni ushindi na hakuna jambo lingine, mashabiki watupe sapoti," amesema.

Leo, Uwanja wa Sokoine Mbeya City itaikaribisha Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic