Eymael amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na kila mchezaji anatimiza majukumu yake mazoezini jambo linalompa nguvu ya kuamini kwamba atapata matokeo mazuri.
"Wachezaji wanaonyesha ari na nia ya kupambana kwa ajili ya timu, ligi ina ushindani mkubwa na kila timu inahitaji matokeo hata sisi pia tunahitaji ushindi," amesema.
Yanga ikiwa imecheza mechi 17 imepoteza mechi tatu ambapo ya kwanza kupoteza ilikuwa mbele ya Ruvu Shooting kwa kuchapwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment