February 25, 2020


NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa wamekubaliana kuendeleza vita ya kuuwinda ubingwa mpaka tone la mwisho kutokana na morali waliyonayo wachezaji huku wakiwataka wapinzani wao Simba wasifikiri kazi wamemaliza ndani ya ligi.
Abdul amesema kuwa bado wanaendelea kupambana kufikia malengo waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kutwaa kombe la ligi kwani bingwa bado hajajulikana.
“Ushindani kwenye ligi ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi jambo hilo linatufanya nasi tuzidi kupambana kufikia malengo ambayo tumejiwekea, hatujakata tamaa kufikia malengo yetu ya kuleta ushindani wa kutwaa ubingwa kwani bado tuna mechi za kucheza ambazo tuna imani tutafanya vizuri,” amesema Abdul
Ally Mtoni ‘Sonso’ beki wa Yanga amesema kuwa wachezaji bado wana morali ya kupambana jambo ambalo linawapa nguvu ya kuamini kwamba nafasi ya kutwaa ubingwa ipo.
“Hatujamaliza kazi kwa sasa bado tunaendelea kupambana kikubwa ni kuona namna gani timu itapata matokeo kabla ya kuanza kufikiria ubingwa, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

6 COMMENTS:

  1. Masikini Roho zao kwa hakika wanatia huruma Sana hasa kutokana na wanayoyasema utafikiri wanaweseka. Poleni sana

    ReplyDelete
  2. Ni kweli brother,maana hata man city bado wanajipa matumain yakutwaa ubingwa,kazaneni maana bado kuna viporo mkijichanga na hizo pwent mojamoja mnachukua ubingwa,mabingwa wa jadi au mabingwa wa kihistoria,timu ya wananchi haya ni majina mnayojiita pale tu mnapokua katika hali tete ya aina yoyote,ikitokea mmeshinda vijimechi vyakuotea mnajiita young african sport club,poleni sana kila mtu avune alichopanda huu ni wakati wa mavuno.

    ReplyDelete
  3. tumia busara bro unaposema gongowazi unamtukana kila aliye fukara ambae hana uwezo wa kupata shati zuri au jipya na katika dunia kuna kupanda na kushuka na tambua kua aliekupa wewe ndie alieninyima mimi (chunga sana kauli yako) !!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmesahau mlivyoita mashabiki wa simba vibaka kwa sababu tu tapeli mmoja kaleta wazungu uwanjani wakiwa na jezi za wananchi
      mkajiona mashabiki wote wa yanga mmekuwa wazungu! Mkuki kwa kunguruwe...

      Delete
    2. Kaka pamabana na hali yako haya mengne ya maisha tunamuachia mola lakini kimpira ninyi ni gongowazi kwani mmeita mashabiki wa simba majina ya kila aina nadhani ni zamu yenu. mpaka mnadiliki kusema simba ni timu ya mashetani je ninyi ni wakamilifu ohoooooo inapenyaaaaaaa gongowazi mpooooooo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic