March 11, 2020

NICOLAS Musonye aliyekuwa Katibu Mkuu wa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) amesema kuwa ameridhia kuachia ngazi hiyo na kumtakia kila la heri Mkurugenzi Mtendaji Aeuko Geucho.

Musonye alidumu kwenye nafasi hiyo kwa miaka 21 amesema kuwa amefaya kazi kwa ushirikiano mkubwa na Tanzania na ana imani ya kuendelea kutoa ushirikiano kwa kiongozi mpya.

Akizungumza na Saleh Jembe, Musonye amesema kuwa kulikuwa na chokochoko nyingi na mambo mengi aliyopitia ila alikomaa na kufanya kwa ukakamavu.

"ilikuwa ni siasa inapigwa na chokochoko zikwa nyingi mwisho wa siku nimemaliza salama, nimeridhia kuachia ngazi na nitaendelea kutoa ushirikiano kwa uongozi mpya," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic