March 11, 2020


KIKOSI cha Simba leo kimeibuka na ushindi wa mabao 8-0 mble ya Singida United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Simba iliingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 na Yanga huku Sinigida United ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 2-1 na Tanzania Prisons jambo lililofanya timu zote zcheze kwa kukamiana.

Meddie Kagere alifunga mabao manne kwenye mchezo wa leo ambapo alifungua pazia dakika ya 1 kwa pasi ya Tshabalala, dk 25  baada ya kukutana na mpira uliotemwa na kipa dk ya 41 na dk 71 kwa pasi ya Dilunga.

Mengine mawili yalifungwa na Deo Kanda dk 12 kwa pasi ya Kapombe,na dk ya 18 pasi Bocco, John Bocco alifunga bao moja dk ya 19 na Sharaf Shiboub alifunga bao moja dk 59 kwa pasi ya Deo Kanda.

Singida United ilimaliza ikiwa pungufu baada ya mchezaji wao Haruna Moshi 'Boban' kuonyeshwa kadi nyekundu dk 52 kwa kumpiga kiwiko Manula.


Ushindi huo unaifanya Simba kuwa nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 71 baada ya kucheza mechi 28 huku Singida United ikiwa nafasi ya 20 baada ya kucheza mechi 28 na ina pointi 12.

6 COMMENTS:

  1. Wamenunuliwa mechi ili kuwaziba mdomo wapenzi. Ogopa sana watu walio kibiashara. Ata Yanga kesho msipojipanga mnafungwa ili jamaa wapate furaha. Jamaa wanatuulia mpira wetu bongo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ushamba wewe, Yanga wangekuwa wazuri wamefanya nini kimataifa kama di kubebwa tu miaka yote

      Delete
    2. Unanunua mechi siku zote nani hajui hilo

      Delete
  2. Yanya ni mamama tu hawana jipya hata wakibebwa wanataka kununuliwa gagulo, Simba iliwbeba championi league wakasema haikuwa lengo lao , mtaishia kusema kama mamama tuu , hamna jipya subiria tu labda manji akirudi na malinzi

    ReplyDelete
  3. March 8 ilionyesha Nani kidume, mbona hawakushida mbele ya wanaume.
    Kitumbua kishaingia mchanga,ndio Basi tena.
    Nisawa na mke kupigwa na mumewe akalipiza wa house girl.

    ReplyDelete
  4. Simba we are good enough thank you for what you have done yesterday so keep it up but i was stare why not at least 10 goal what I can say apart from our win yesterday problem remain to our team there is no competitive sprit and match featness is low I don't know there more ruxury to our player than featness exercise but we thank omnipotent from what Simba you did for us that enough keep it up

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic