March 11, 2020

MUUAJI wa Simba kwenye mechi ya watani wa jadi, Bernard Morrison amesema kuwa shangwe za mashabiki wa Yanga zilimpa nguvu ya kupambana kwa ajili ya timu na mashabiki pia.

Kiungo huyo raia wa Ghana aliifungia bao timu yake ikiwa ni mchezo wake wa Kwanza wa dabi baada ya kutua Bongo kuitumikia timu hiyo kwenye dirisha dogo.

Morrison amesema kuwa wingi wa mashabiki na kelele zao mwanzo mwisho zilimpa nguvu ya kupambana na kuifungia bao la ushindi timu yake. 


"Kelele za mashabiki zilikuwa na nguvu kwangu na timu kiujumla, zimenifanya niwe na furaha na ninaamini wanahusika Kwa kiwango kikubwa kwenye ushindi wetu tulioupata mbele ya Simba," amesema .

Yanga ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50 imecheza mechi 25 huku mkononi ikiwa na mechi mbili kuwa Sawa na vinara Simba waliocheza mechi 27 na pointi 68.

1 COMMENTS:

  1. Na leo yanga kama wanaweza wafunge simba ili wapunguze point

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic