March 13, 2020


NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa sababu iliyowafanya wakapoteza mbele ya KMC ni kubadilishiwa uwanja uliopangwa kuchezwa awali jambo lililowaathiri kisaikolojia.

Awali mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru Machi 12 na Yanga kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 ulipaswa uchezwe Uwanja wa Taifa.

"Tulikuwa tunajua kwamba tutacheza Uwanja wa Taifa ila tukaambiwa kwamba mchezo utachezwa Uhuru jambo hilo kiasi chake limetufanya saikolojia isiwe sawa, lakini kwa kuwa ni mpira matokeo tumeyakubali na tunawapongeza wapinzani kwa kutumia nafasi moja waliyoipata," amesema.

 Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo imepoteza mechi nne baada ya kucheza mechi 26 kwenye Ligi Kuu Bara.

5 COMMENTS:

  1. Kwahivo kama Ada yenu mmeonewa. Timu yenu mbovu na kila mkifanya panic mnazidi kuanguka. Jee bado mnazo nguvu za kuikebehi Simba ambayo 99% ubingwa ni wao kwa kigoli cha kulimbukiza. Simba pia Mara nyingi hubadilishiwa viwanja lakini hatuwasikii kulalamika.

    ReplyDelete
  2. Ule uwanja mwingine walitegesha uchawi wao amba ulishindwa kufanya kazi uwanja wa Uhuru

    ReplyDelete
  3. jikazeni acheni visingizio mbona mlipata nafasi nyingi lakinilishindwa kuzitumia. pia wachezaji walicheza chini ya kiwango

    ReplyDelete
  4. Kutoka uwanja wa sokoine kwenda samora ilikuwa poa
    Yanga bwana mmethibitisha msemo huu'maiti ya kiswahili hailosi sababu"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic