March 21, 2020



YUSUPH Mhilu, mshambuliaji wa Kagera Sugar amesema kuwa kwa sasa hayupo Bukoba baada ya timu kuvunja kambi ameamua kutimkia kijijini Rufiji ili kujilinda na Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu mwenye mabao 11 na pasi mbili za mabao ambaye malengo yake makubwa ni kuona anatwaa tuzo ya kiatu cha ufungaji bora kilicho mkononi mwa Meddie Kagere wa Simba.

“Kwa sasa kambi tumevunja nami sipo Bukoba nipo Rufiji nikiendelea kuchukua tahadhari ya virusi vya Corona, maombi yangu kuona hali hii inatulia na kila kitu kinarejea kwenye hali yake ya kawaida,” amesema Mhilu. 

Kagere kwa sasa ni kinara wa kucheka na nyavu, ametupia mabao 19 kwenye Ligi Kuu Bara, msimu uliopita wa 2018/19 alitupia mabao 23.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic