ANAANDIKA Haji Manara,kupitia ukurasa wake wa Instagram Ofisa Habari wa Simba:-Heri neno kavu na utulivu kuliko karamu ya Mfalme na machafuko ‘Bible’.
"Nilikwenda mwenyewe mchana huu klabuni Yanga,bahati mbaya sana sikuwakuta viongozi wa klabu. Wazee niliowakuta nje baada ya kuwaeleza nimekuja kukabidhi pesa za masimango walinisihi sana nisifanye hivyo na wakaniambia yule ni mgeni hapa mjini na hajui tamaduni zetu na kuniomba nisirejeshe hata thumuni.
Nimefundishwa kuwatii wazee, na ntarejea kwa Wanasimba walionikabidhi pesa zao,busara itawashauri tupeleke hospitali kwa wagonjwa wasiojiweza,ikiwapendeza tutafanya hvyo!
Kwetu nimefundishwa uungwana,kwetu nimepata malezi bora,kwetu wazazi wangu walinijaza na jeuri ya kutokubali kuonewa wala kunyanyaswa. halaf mm sijatoka Mbwinde,,hilo ni Muhimu sana na ndio maana naweza kuwa Msemaji pekee naweza kwenda klabu nyingine tena mchana kweupeeeee.
Binamu yangu Haji;siku hizi vilabu vyetu vimevamiwa na watu wasiojua utani wa Yanga na Simba.Nakumbuka miaka ya zamani kuja hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 wazee wetu walikuwa wanakaa pamoja baada ya mechi na ikitokea timu moja imeshinda basi washindi walikuwa wanawanunulia washindwa kahawa hadi pilau katika hali ya kunogesha utani ilihali wakiwa wamekaa pamoja huku wakichachurana kwa kila tambo.Lakini baada ya hivi vilabu kuvamiwa na watu wasiojua utani wa Simba na Yanga imekuwa ni kinyume na ilivyokuwa miaka ya nyuma.Hebu wape story za enzi hizo hali ilivyokuwa baada ya mechi pale maeneo ya Mwembe Yanga Temeke,Shibam hotel na Butiama hotel Magomeni,Manzese msufini au hata uwanja wa Karume.Kulikuwa na ushabiki wa kutaniana ilhali watu wamekaa pamoja huku upande ulioshindwa ukilazimishwa kunywa birika la kahawa na kashata zilizonunuliwa na washindi lakini siku hizi hali ni tofauti kabisa mtu anakurupuka toka kijijini kwao akifika Dar basi anajifanya yeye ndo mjuaji wa kila kila kitu.
Pole kaka mwenye asili haachi asili ukishindana na mpumbavu na ww utaonekana moumbavu achana na huyo mpumbavu ni maana alifukuzwa yanga namshukuru rais kwa kumpa hiyo kazi ya dc
Utani wa Simba na Yanga umepotea kabisa baada ya "wakuja" wengi kuvamia ushabiki wa hizi timu.Siku hizi unaweza hata kutolewa roho kwa kushabikia hizi timu.Zamani mechi unabisha tunataniana maisha yanaendelea.Tulikuwa tunataniana kwenye misiba ,kwenye harusi na kushirikiana kwenye ugonjwa. SIKU hizi mashabiki uchwara wamegeuz timu hizi vijiwe vya chuki husuda na uzushi.
Haji manara ni mgonjwa wa akili,anataka atanie wenzake tu, yeye akitaniwa anakasirika,lazima ajifunze kua hutani hauitaji hasira,simba wakina dalali waliitania yanga hata kwenye msiba wa mzee akilimali,mbona hakuna mtu aliyeita masimango,Haji manara acha ushamba,km huuwezi utani kaa kimya.
Binamu yangu Haji;siku hizi vilabu vyetu vimevamiwa na watu wasiojua utani wa Yanga na Simba.Nakumbuka miaka ya zamani kuja hadi mwishoni mwa miaka ya 1980 wazee wetu walikuwa wanakaa pamoja baada ya mechi na ikitokea timu moja imeshinda basi washindi walikuwa wanawanunulia washindwa kahawa hadi pilau katika hali ya kunogesha utani ilihali wakiwa wamekaa pamoja huku wakichachurana kwa kila tambo.Lakini baada ya hivi vilabu kuvamiwa na watu wasiojua utani wa Simba na Yanga imekuwa ni kinyume na ilivyokuwa miaka ya nyuma.Hebu wape story za enzi hizo hali ilivyokuwa baada ya mechi pale maeneo ya Mwembe Yanga Temeke,Shibam hotel na Butiama hotel Magomeni,Manzese msufini au hata uwanja wa Karume.Kulikuwa na ushabiki wa kutaniana ilhali watu wamekaa pamoja huku upande ulioshindwa ukilazimishwa kunywa birika la kahawa na kashata zilizonunuliwa na washindi lakini siku hizi hali ni tofauti kabisa mtu anakurupuka toka kijijini kwao akifika Dar basi anajifanya yeye ndo mjuaji wa kila kila kitu.
ReplyDeletePole kaka mwenye asili haachi asili ukishindana na mpumbavu na ww utaonekana moumbavu achana na huyo mpumbavu ni maana alifukuzwa yanga namshukuru rais kwa kumpa hiyo kazi ya dc
ReplyDeleteUtani wa Simba na Yanga umepotea kabisa baada ya "wakuja" wengi kuvamia ushabiki wa hizi timu.Siku hizi unaweza hata kutolewa roho kwa kushabikia hizi timu.Zamani mechi unabisha tunataniana maisha yanaendelea.Tulikuwa tunataniana kwenye misiba ,kwenye harusi na kushirikiana kwenye ugonjwa. SIKU hizi mashabiki uchwara wamegeuz timu hizi vijiwe vya chuki husuda na uzushi.
ReplyDeleteHaji manara ni mtani jembe asiyetaka akufilie mbali,hakuna mtani anaweza kyfanya vile ambavyo amekua anafanya manara huo ndio utani original.
ReplyDeleteMmeongea maneno ya busara sana. Ushabiki si uadui. Huu utani wa jadi wa Yanga na Simba uendelee kuwa chachu ya mandeleo ya soka Tanzania.
ReplyDeleteHaji manara ni mgonjwa wa akili,anataka atanie wenzake tu, yeye akitaniwa anakasirika,lazima ajifunze kua hutani hauitaji hasira,simba wakina dalali waliitania yanga hata kwenye msiba wa mzee akilimali,mbona hakuna mtu aliyeita masimango,Haji manara acha ushamba,km huuwezi utani kaa kimya.
ReplyDelete