March 7, 2020


NYOTA watatu wa Azam FC walioongeza mkataba ndani ya klabu hiyo wamesema kuwa watapambana kufikia malengo waliyojiwekea pamoja na yale ya klabu kiujumla.

Azam FC imewaongezea kandarasi ya miaka mitatu nyota wake watatu ambao ni Lusajo Mwaikenda, Oscar Masai ambao ni mabeki na Andrew Simchimba ambaye ni mshambuliaji.

Dili hilo  la nyota hao watatu wanaokipiga Azam FC litameguka mwaka 2023.

Simchimba ambaye ni mshambuliaji amesema kuwa ataendelea kupambana kwa juhudi ili kutimiza malengo ya klabu pamoja na yale aliyojiwekea.

Masai ambaye ni beki amesema kuwa nidhamu na juhudi ni vitu atakavyoendelea kuvifanyia kazi zaidi.

Lusajo abaye ni beki amesema kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuyafikia malengo yake pamoja na timu hivyo ataendelea kupambana.

 CEO wa Azam FC, Abdulkarim Amin Popat amesema kuwa sababu kubwa ya kuwapa dili nyota hao ni kuendeleza vipaji vya vijana pamoja na kufuata maombi ya benchi la ufundi ambalo limekubali uwezo wa nyota hao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic