SIMBA leo itakuwa na kazi ya kumenyana na Singida United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00 jioni.
Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Simba ilishinda kwa bao 1-0 lililopachikwa kimiani na Miraj Athuman aliyemalizia pasi ya Mzamiru Yassin.
Uongozi wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya kuzisaka pointi tatu baada ya kupoteza mbele ya Yanga mchezo uliopita kwa kufungwa bao 1-0.
Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kuendeleza kutoa burudani na kupata ushindi mbele ya wapinzani wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment