LIGI kuu Bara sasa inazidi kusonga mdogomdogo ikipaga hatua ndefu na fupi kwa kila timu kupata kile ambacho wakuwa wamekipanda na wanastahili kukivuna.
Kila timu kwa sasa inatazama upepo wake namna unavyokwenda ili kupata matokeo chanya yatakayoifanya ibaki kwenye nafasi inayofikiria kuwepo.
Ushindani ni mkubwa ila kumekuwa na kilio kwamba bado kuna ugumu wa kuendesha ligi kwa sasa kwa baadhi ya timu kutokana na suala la ukata ambao unazikumba baadhi ya timu.
Hali hii ni mbaya iwapo kuna timu ambazo zinapitia kipindi kigumu na zinafikiria kupata matokeo changamoto hii inapaswa ifanyiwe kazi ili timu zipate nafasi ya kuendelea kuleta ushindani kwenye ligi
Kwa nyakati hizi za lala salama Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linapaswa liongeze umakini na kutazama mianya ilipo kwa zile timu ambazo zinadai kuzidiwa na kutoa sapoti haina maana fedha ndio sapoti wakati mwingine hata mawazo ya namna ya kujiinua hapo ni mchango mkubwa.
Ipo hivi kwa sasa kila timu imeshapiga hesabu zake na kuona kile ambacho inastahili kukivuna baada ya kuvuna kwenye michezo yao iliyopita ambayo wamecheza.
Tunaona kila mmoja anapambana na hali yake hilo ndilo linahitajika cha msingi ni kujua ni kwa namna gani inapambana ili kupata matokeo uwanjani?
Kuna umuhimu pia kwa wachezaji kuongeza umakini wawapo ndani ya uwana kwa kulinda haki za mchezaji wa timu pinzani mpira sio vita bali ni burudani.
Matumizi ya nguvu nyingi ndani ya uwanja hayana faida kwani kinachomata ndani ya uwanja ni mbinu na akili za mpira kwa wachezaji kufuata maelekezo waliyopewa na mwalimu wakati wa mafunzo.
Pia dharau zimekuwa nyingi kwa kuwa hakuna ambaye anajali hivyo kwa kuanza mmejitahidi itawafanya wengine kuhofia kufanya maamuzi ambayo hayatazingatia sheria 17 za mpira.
Waamuzi wamekuwa wanafanya maamuzi yao kwa kuwa hakuna aliyekuwa anawafuatilia na hata kama wanafuatilia basi walikuwa wanachelewa kutoa maamuzi hali iliyokuwa inaongeza kiburi.
Timu nyingi zinacheza mechi ambazo hazirushwi na Azam TV hili ni baya kutokana na rekodi zao kuwa mbaya pindi wanapochezesha mechi za aina hii na ushahidi kukosekana hasa kwa wale ambao wataamua kutoa malalamiko yao.
Hivyo rai yangu kwa TFF kuwa macho muda wote kwenye mechi hizi ambazo kila mmoja anapigania timu yake ipate matokeo bila kujali anacheza na nani na katika wakati gani hilo hajui zaidi ya kutazama matokeo chanya kwakwe.
Mechi za ugenini kwa sasa zinakuwa ngumu kwa timu zote kutokana na kuwepo kwa kampeni ya kila timu ishinde mechi zake za nyumbani hili ni gumu na baya kwenye soka letu kwani halileti ushindani bali linazalisha chuki.
Hakuna ambaye anapenda kupata matokeo mabaya kwenye michezo yake ya mwisho hali inayofanya wengi kulazimisha mambo ambayo wanayatarajia kutokea hili halijakaa sawa.
Kwa mechi ambazo hazitarushwa mojakwamoja wapelekwe waamuzi maalumu ambao watakuwa wanakusanya ripoti na kutoa taarifa kwa wakati na sio baada ya muda kupita italeta mvurugano kwenye ligi na kupoteza ladha ya ushindani.
Ili kuepukana na maamuzi haya TFF ni lazima iwafuatilie waamuzi kwa ukaribu hatua kwa hatua na kutoa maamuzi hapohapo na sio kuwafungia macho wanaua soka letu kwa mapenzi yao binafsi.
Sheria 17 lazima zifuatiliwe na viongozi wa timu wanapaswa wakomae kwenye maandalizi na sio kutaka kushinda nje ya uwanja hili halipo sawa ndio maana tunapata timu ambazo zinashindwa kufika mbali.
Kupitia sheria za mpira ni rahisi kumpata mshindi wa haki na itafanya hata Yule anayeshindwa kukubali makosa yake na sio kuanza kutafuta sababu ya kushindwa.
Kuna timu ambazo kwa sasa zimeanza kupoteza matumaini ya kubaki kwenye ligi nina imani bado nafasi ya kurekebisha makosa ipo na iwapo zitaamua kufanya tofauti na mwanzo.
Kila mkoa kwa sasa naona kumekuwa na kampeni ya kutaka kuona timu zao zinashnda michezo yao yote hii ni mbaya na inaua ushindani waziwazi waache timu zishinde kwa kupambana.
Kama kuna timu ambayo inapanga matokeo kwa njia zake za ujanjaujanja ikibainika inatakiwa ichukuliwe adhabu kali na iwe mfano kwa timu nyingine zenye tabia kama hiyo ziache mara moja.
Vita imekuwa kubwa ndani ya ligi ambapo tunaona ufalme wa ubingwa na ufalme wa kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara umekuwa mkubwa kwa timu zote kutafuta matokeo.
Kwa timu itakayoshuka daraja tunatarajia kuona inashuka ikiwa kweli imeshindwa yenyewe kihalali na sio kwa kuonewa italeta matatizo.
Uzuri ni kwamba mchezo wa mpira ni mchezo wa wazi hivyo hakuna ambaye anaweza kudanganya kwamba alishindwa kupata matokeo chanya uwanjani.
TFF msijisahau na kuchangua aina ya timu kwa ajili ya kuzitazama kwa ukaribu na kujenga matabaka itavunja ushindani kwenye ligi yetu ambayo kwa kiasi chake imeanza kuwa na ushindani.








0 COMMENTS:
Post a Comment