KIUNGO wa Klabu ya Real Madrid, Casemiro amefunguka kuwa anapenda kucheza na staa wa PSG, Neymar Jr atafurahi akiwa ndani ya klabu hiyo msimu ujao.
Neymar ni mchezaji ambaye msimu uliopita alikuwa akitikisa katika usajili wa Ulaya kuwa huenda atarudi katika klabu yake ya zamani ya Barcelona.
Casemero anacheza pamoja na Neymar kwenye timu ya Taifa ya Brazil anatamani staa huyo ajisogeze katika Uwanja wa Santiago Bernababeu.
"Nataka Neymar aje kujiunga na Real Madrid, huwa naongea naye karibu kila siku kuhusu suala hilo sababu yeye ni mchezaji mkubwa na ana uwezo," amesema.








0 COMMENTS:
Post a Comment