DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa kazi bado ipo kwenye Ligi Kuu Bara kwani kuna mechi nyingi za kucheza ambazo wanatakiwa wapate matokeo ikiwa ni pamoja na mechi yao dhidi ya Simba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Nchimbi mwenye mabao sita ndani ya ligi amesema kuwa wamekuwa wakipewa maelekezo ya kufanya na mwalimu jambo ambalo linawapa morali kubwa ya kufanya wakiwa uwanjani.
“Mwalimu amekuwa akituelekeza mambo mengi ya kufanya nasi tunayafanyia kazi, ila mambo bado kwani tuna mechi nyingi na ngumu ikiwa ni pamoja na mechi yetu dhidi ya Simba.
“Kwa sasa akili zetu ni kwenye mechi zetu za mbele tunahitaji kupata pointi tatu na hilo linawezekana kwa kuwa tunashirikiana,” amesema Nchimbi.
Machi 8, Uwanja wa Taifa Yanga itaikaribisha Simba ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 mchezo wa kwanza uliochezwa Januari 4,2020.







Mnyama hivohivo Bila ya majisifu na Bila ya kelele na muwashituze kwa kichapo watulie. Hivi sasa wana panic na itakuwa ndio mwisho wa kuuota ubingwa
ReplyDelete