UONGOZI wa Biashara United umesema kuwa kwa sasa bado wanaendelea kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona na watarejea kambini pale Serikali itakapotoa tamko.
Wachezaji wa Biashara United kwa sasa wamekwama kuendelea na mazoezi baada ya kambi kuvunjwa baada ya tamko la Serikali kuzuia mijumuiko isiyo ya lazima Machi 17,2020.
Tamko hilo litaendelea baada ya Serikali kutoa taarifa, Aprili 14 kwamba zuio la mijumuiko lipo palepale mpaka watakapotoa tamko kutokana na maambukizi ya Virusi kuendelea kuwepo nchini.
Mwenyekiti wa Biashara United, Selemani
Kichele amesema: “Tumekaa na kujadili tukakubaliana tuendelee kusubiri tamko la
Serikali juu ya Corona, wakitangaza tuendelee na michezo sisi tutawaita
wachezaji kambini kuendelea na kambi lakini kwa sasa wachezaji wapo nyumbani.”







0 COMMENTS:
Post a Comment