April 15, 2020


UONGOZI wa Simba umesema kuwa hakuna timu itakayomchomoa nyota wao raia wa Zambia kwa sasa, Clatous Chama kutokana na kuhitaji huduma yake.

Kumekuwa na mvutano mkubwa kwa sasa kuhusu Chama kati ya mabosi wa Simba na Yanga ambao wanaelezwa kuiwinda saini yake huku Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela akieleza kuwa wamejiweka pembeni kuhusu suala hilo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema:"Hakuna ambaye anaweza kututisha kwa sasa kuhusu kumpata nyota wetu Chama, tunamhitaji na tunamkataba naye hivyo ikiwa timu inamtaka ni lazima ijipange na ifuate utaratibu tofauti na hapo lazima tutawashtaki,".

Taarifa ambayo imetolewa kupitia Ukurasa wa Istagram wa Simba imeeleza kuwa Chama amesema kwamba bado ana mkataba na Simba.

Mwakalebela amesema kuwa utaratibu wa usajili anautambua na alifanya hivyo kwa lengo la utani hivyo anaomba msamaha kwa uongozi wa Simba na mashabiki kiujumla.

"Tunajiweka pembeni katika suala hili hii ni kutokana na awali kuwa na mkanganyiko kidogo lakini ilikuwa ni sehemu ya utani, kwa sasa acha maisha yaendelee," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Mwakalebela ukome kidandia mambo, usione vinaelea, vinaundwa

    ReplyDelete
  2. Kwani Simba tulipo wafungeni bao moja nunge huyo chama hakuepo..C alifunikwa na fei toto hadi akawa anafanya rafu za kijinga,chama c mchezaji hana uwezo wa kumzidi fei toto

    ReplyDelete
  3. Kumbe woga kama kunguru. Si mnajinadi kuwa mmeambiwa mchezaji yoyote mnaemtaka kwa thamani yoyote Mtaletewa tu mkawa mnaweseka kumbe mmetiwa mtegoni na sasa mnapapatika kama Samaki alietolewa Bahraini. Cheza na Mnyama

    ReplyDelete
  4. Mimi Yanga lakini kumlinganisha Chama na Fei Toto ni utoto.Chama kafanya mengi kwenye soka bila ushabiki. Fei Toto kafanya nini cha maana?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic