April 7, 2020


INAELEZWA kuwa uongozi wa Simba upo kwenye mazungumzo na nyota wao wa zamani, Emannuel Okwi ili arejee tena kukipiga kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Okwi kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya Al Ittihad alijiunga nayo kwa dau la dola 257,000 zaidi ya shilingi milioni 592 akitokea Simba.

Habari zinaeleza kuwa kinachokwamisha dili la nyota huyo kwenda sawa ni mkwanja ambao anauhitaji kuwa mkubwa jambo ambalo linawapasua kichwa mabosi wa Simba.

"Okwi anatakiwa kurudi ndani ya Simba ila ishu kubwa ni mshahara wake ambao anahitaji kulipwa zaidi ya milioni 20 kwa mwezi jambo ambalo bado linajadiliwa.

"Mahitaji yake ni kuona analipwa dola 10,000 (zaidi ya milioni 23) kutokana na hali hiyo uongozi umeona uweke kando kwanza dili hilo," ilieleza taarifa hiyo.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa  amesema:" Kwa sasa kocha ametoa mapendekezo yake ya mchezaji wa kusajiliwa na kuachwa, hatuwezi kuweka wazi siri za klabu muda ukifika kila kitu kitajulikana,".

Okwi akiwa Simba ametwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara tatu ikiwa ni msimu wa 2011/12,2017/18 na 2018/19.

Chanzo SpotiXtra

6 COMMENTS:

  1. Okwi hana thamani hiyo simba waachane nae. Asifanye simba ni sehemu ya kuchuma mihela na kwenda kutumbua uganda. Umri na uwezo wake kwa sasa hawezi kulipwa hela zote hizo. Ni dhihaka kwa wazawa

    ReplyDelete
  2. Wazawa wajitume mpira nimchezo wa wazi wapi mchango wa Ajibu, bocco au ndemla

    ReplyDelete
  3. Viongozi wetu huwa nawashangaa sana wachezaji wako wengi sana,wanahangaika na mtu meenye umri kama wangu.

    ReplyDelete
  4. Nahauri waachane nae hana thaman hiyo wachezaji wazuri wapo wengi

    ReplyDelete
  5. Enter your comment...mbona habari hiyo hamsemi ni ya uongo iv mikia umbumbu mtaacha lini,yan ingekuwa stori ya morison kuhusu kuwafunga,au yanga kumtaka chama lazima mchonge yan hii habari imeizungumzia simba tu naona mmefurahi saaaaana dooooooh mbn hamumkosoi Salehjembe leo,au leo yuko sahihi,mbn hamuhoji iz habar kazitoa wapi maana kila siku mnamfokea,

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha ukazuzu mbona kila jambo uingize ushabiki? unaboa kama hawasemi yanakuhusu? acha watu watoe maoni yao kwanza ukipenda soma usipopenda kaa pembeni sio kila jambo morrison au ni dawa ya Corona tumeona mafundi wengi mno kwan huyo kafanya lipi yanga mpaka kutukuzwa kiasi hicho unaboa ebo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic