April 16, 2020

JAMES Kotei, kiungo mkabaji ambaye alicheza kwa mafanikio ndani ya Klabu ya wa Simba amesema kuwa anapenda kurudi ndani ya Simba kwa kuwa hakuzinguana na viongozi wakati akicheza msimu uliopita kabla ya kutimka jumla.

Kocha wa wakati huo aliyekuwa naye Kotei ndani ya Simba Patrick Aussems alisema kuwa alikuwa anahitaji huduma ya Kotei ila mambo yalikuwa magumu kwani ilishindakana kubaki.

"Miongoni mwa wachezaji ambao nilikuwa nahitaji kupata huduma yao alikuwa ni Kotei ila ninadhani uongozi ulimpa ruhusa kuondoka katika hilo siwezi kuingilia," alisema Aussems kabla ya kuchimbishwa.

Kotei ambaye baada ya kutimka Simba alikipiga Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na kwa sasa yupo ndani ya Belarus amesema: "Uzuri ni kwamba viongozi wa Simba pamoja na wachezaji wote ni familia, ninapenda kuwa sehemu ambayo ninakuwa na furaha sioni shida kurudi tena iwapo mambo yatakuwa safi.

"Kazi ya mchezaji ni kucheza hilo lipo wazi nami pia ni mchezaji popote kwangu nakipiga,".

2 COMMENTS:

  1. Rejea nyumbani tutakupokea kwa vigelegele. Simba ipo moyoni mwako

    ReplyDelete
  2. NYIE VYOMBO VYA HABARI NDIO MNAZUSHAZUSHA MAMBO NA TETESI ZA UONGO HALAFU BAADAYE VIONGOZI WA KLABU WANAINGIZWA MKENGE KUJIBU TETESI....HEBU ACHENI MARA MOJA KAMA HAKUNA HABARI NYINGINE ELIMISHENI RAIA KUHUSU CORONA NA NAMNA YA KUJIKINGA KULIKO KUTAFUTA UMBEA NA UONGO KWENYE USAJILI ILI KUMKUZA MCHEZAJI NA KUZIINGIZA KLABU KWENYE NAFASI YA KUKANUSHA AMA KUTETEA HABARI...ILI WAONGOPE NA KUTOA KAULI HALAFU WAINGIE KWENYE MATATIZO


    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic