April 3, 2020


ADOLF Rishard, Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons amesema kuwa kwa wakati huu tuliopo ni muhimu kwa watanzania kuzidisha dua ili nchi itoke kwenye janga hili la Corona na dunia nzima kiujumla.

Kwa sasa Ligi Kuu nyingi duniani zimesimamishwa kupisha maambukizi zaidi ya Virusi vya Corona ambavyo wataalamu wanaeleza kuwa vinaenea kwa njia ya hewa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Rishard amesema kuwa ni wakati wa kuungana kwa watanzania wote kufanya dua ili nchi ipone.

"Muhimu kwa kila mmoja kufanya dua na kuungana kwa pamoja kupambana na Virusi vya Corona kwani hili ni janga la dunia kiujumla hivyo ni muhimu tukiungana," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic