ZINEDINE Zidane anatajwa kuwa ndiye kocha bora ndani ya Klabu ya Real Madrid, lakini ubora wake siyo kwenye kufundisha tu, bali na kuvumbua vipaji vya wachezaji wengi.
Zidane
amekuwa na ile pua nzuri ya kunusa vipaji ambavyo vimepata nafasi ya kuonyesha
uwezo wao na hii ni baada ya kutambua uwezo wao mapema.
Kuna vipaji
sita ambavyo amevivumbua na ikawa faida kwa Klabu ya Real Madrid. Kwa sasa pua
yake inaonekana kunusa kwa dogo wa miaka 17 anayeichezea Rennes ya Ufaransa,
Eduardo Camavinga.
Wakati wa
uchezaji wake soka, Zidane alikuwa fundi kweli, akaja kwenye ukocha anafanya
vizuri, lakini sasa anatajwa kuwa mmoja wa maskauti wazuri.
Timu yake ya
mwisho kuichezea ilikuwa Madrid ambayo alianza kuichezea 2001, hadi 2006.
Mwaka 2014
akaanza rasmi ukocha akianzia timu ya vijana ya Real Madrid, kisha 2016 hadi
2018 akaifundisha timu ya wakubwa, akaondoka na kurudi 2019 ambapo yupo hadi
sasa.
Baadhi ya
nyota ambao Zidane ambaye ni mtu anayeheshimika ndani ya Real Madrid amewaibua
na leo hii wanatamba, ni hawa hapa:
Kylian Mbappe
Ni miaka
saba sasa Zidane amekuwa akipambana kutaka kuhakikisha Kylian Mbappe anatua ndani
ya viwanja vya Santiago Bernabeu.
Zidane
alianza kumsaka Mbappe akiwa mdogo katika Kituo cha Kukuza Soka cha Monaco.
Katika hilo
akishirikiana na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, bado wanapambana kuona
wanamsajili haraka iwezekanavyo.
Mbappe, 21,
kwa sasa anakipiga PSG, mwaka 2012 Zidane aliomba asajiliwe ndani ya Real
Madrid.
Baada ya
kushindwa kusajiliwa, Mbappe alinukuliwa akisema: “Sikutaka kwenda Madrid kwa sababu
nilitaka kubaki ndani ya nchini yangu.”
Mwaka 2017,
Mbappe akaibuka kuwa Mchezaji Bora Ulaya mwenye umri mdogo akiwa na miaka 18.
Madrid
wakaanza mazungumzo na familia yake ili kuona wanafanikiwa kumsajili dogo huyo
na mpaka sasa bado yupo mikononi mwa PSG, ila Zidane bado hajakata tamaa.
Eden Hazard
Msimu uliopita,
Madrid ilimnunua, Eden Hazard kwa kiasi cha euro 100m, lakini ilikuwa atue
kikosini hapo tangu 2009 na Zidane alikuwa anashauriana na rais wa klabu hiyo,
Florentino Perez.
Mwaka 2009, Zidane
aliwahi kusema: “Natamani kumleta Hazard hapa Madrid nikiwa nimefumba macho.”
Lakini
hakukata tamaa, aliendelea kumuwinda mpaka alipofanikiwa kumpata msimu huu.
Hazard sasa
yupo ndani ya Madrid, lakini ameanza vibaya kutokana na majeraha ya mara kwa
mara.
Raphael Varane
Akiwa na
miaka 18, Raphael Varane akiicheza Lens ya Ufaransa, huko ndiko Zidane aliona
uwezo wake, akamsajili kwa kitita cha euro 10m.
Baada ya
kumsajili, Zidane alinukuliwa akisema: “Ni wa kipekee na haikuwa rahisi
kumpata.”
Miaka nane
ndani ya Madrid, Varane amekuwa msaada mkubwa katika safu ya ulinzi na amekuwa
beki bora akicheza sambamba na mkongwe Sergio Ramos.
Fede Valverde
Kiungo huyu
alijiunga na Real Madrid na kuanzia timu ya vijana.
Baadaye
akatengenezwa vizuri na hivi sasa ni msaada mkubwa ndani ya timu hiyo.
Kumbuka
msimu uliopita, Zidane alitaka kumsajili Paul Pogba, lakini ikashindikana.
Akaamua
kumtumia Fede ambaye hajamuangusha kwani amekuwa na msaada kwenye kikosi cha
Madrid.
Zidane
amekuwa akimpenda sana kiungo huyu, anampa nafasi kubwa mbele ya Toni Kroos,
Casemiro na Luka Modric.
Fede
ameibadilisha Madrid msimu huu hasa katika safu ya kiungo hii ni kutokana na
uwezo wake ambao Zidane aliwahi kukiri kuwa pale anapokosekana, timu inayumba.












0 COMMENTS:
Post a Comment