April 20, 2020


YKIPE Gnamien mshambuliaji mwili jumba anayekipiga ndani ya Yanga amesema kuwa kwa sasa anaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona huku akijifua ili Ligi Kuu Bara ikirejea imkute kwenye ubora wake.

Nyota huyo alivunja mkataba ndani ya Klabu ya Gor Mahia ili ajiunge na Yanga kutokana na kupata dili kubwa na mabosi wa Yanga kuelewa uwezo wake.

Kwa sasa ligi imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona inatarajiwa kurejea hivi karibuni pale mambo yatakapokuwa shwari.

Gnamien amesema:"Nina amini mashabiki wa Yanga wanahitaji mambo mazuri nami pia kwa sasa ninajifua ili kuwa bora ligi ikirudi nami nitakua kwenye ubora wangu.

"Mimi nawaahidi mashabiki kufanya vizuri nao pia waendelee kutupa sapoti na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona," .

Ndani ya Yanga ni miongoni mwa 'super sub' kwani bao lake la kwanza alifunga akitokea sub mbele ya Singida United Uwanja wa Namfua kwa bichwa.


2 COMMENTS:

  1. Ndugu muandishi muogope Mungu, kweli Ykipe ni kipenzi cha Yanga? how?

    Au ndio habari za kuungaunga?

    ReplyDelete
    Replies
    1. NDIO NI KIPENZI CHA YANGA,ILA SIO KIPENZI CHA MASHABIKI WA YANGA,ILIHALI HAO NDIO WENYE TIMU,SALEH JEMBE WEWE UMEKUA KAMA FALA NOWDAYS YANI UNAUNGA HABARI ZA UONGO NAKUTUNGA MNGU ANAKUONA BROTHER,UMEKOSA WELEDI YANI UMEPOTEZA SIFA KWA KIPINDI KIREFU SASA,NIKUPE POLE SANA NA UNGETAFUTA SHUHULI ZAKUFANYA NDUGU YANGU.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic