April 16, 2020

Wachezaji wa Mtibwa Sugar kabla ya Ligi kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona

THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa kwa sasa ni muhimu timu zote Bongo kuungana kuongeza nguvu ya kupambana dhidi ya Virusi vya Corona.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Kifaru amesema kuwa kwa sasa dunia inapambana kutafuta njia ya kutokea kwenye Virusi vya Corona.

"Muhimu kwa sasa ni kwa Klabu zote Bongo kuungana ikiwa ni pamoja na Simba, Lipuli, Azam FC na Mwadui katika kupambana na Virusi hivi kutokana na kila mmoja kuwa katika wakati mgumu wa kutafuta njia ya kupona.

"Tupo kwenye wakati mgumu dunia nzima inapambana na kila mmoja anapambana  hivyo ni muhimu kuwa pamoja katika kila hali kwa sasa, tusiache kufuata kanuni za afya pamoja na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic