April 8, 2020

PAUL Nonga, nahodha wa Lipuli amesema kuwa amepata dili la kujiunga na moja ya timu inayoshiriki Ligi Kuu nchini Malaysia mambo yakiwa sawa atasepa Bongo.

Nonga anayekipiga Lipuli amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo ni miongoni mwa wazawa wanaocheka na nyavu akiwa na mabao 11 na pasi nne za mabao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Nonga amesema kuwa kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja umempa nafasi ya kupata timu nchini Malaysia jambo ambalo linampa faraja.

"Ninafurahi kuona kwamba kazi yangu inaonekana na nimepata timu nchini Malysia inashiriki Ligi Kuu nchini humo inaitwa Kuala lumpar FC.

"Muda wa siku 12 nilipata kufanya majaribio na ninashukuru haikuwa mbaya kwani nilionyesha kitu cha kipekee, bado ni mradi endelevu mambo yakiwa sawa nitaweka wazi mipango itakavyokuwa," amesema.

4 COMMENTS:

  1. Waandishi wa zamani walipaswa wafaulu masomo ya lugha, historia na giografia sijui lini malasiya umekuwa ulaya

    ReplyDelete
  2. Huyu jamaa ni mpuuzi sana,yani hapa hakuna mhariri wa habari maana hii blog imekua ikiongoza kwakutoa taarifa za uongo yani ujinga uliokithiri,haina maana kabisa.

    ReplyDelete
  3. Jamani Malaysia iko Asia sio Ulaya. Sio kila nchi iliyoko nje ya bara la Africa iko Ulaya!

    ReplyDelete
  4. malysia iko ulaya toka lini ndiomana kuna Rais mmoja hapa nchini aliwadharau nyie

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic