April 16, 2020


IMEELEZWA kuwa mabosi wa Yanga hesabu zao ni kuibomoa Simba na kuchokomoka na nyota mmoja ambaye amekuwa kwenye ubora wake licha ya kutokuwa na nafasi kikosi cha kwanza kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Kwa sasa mvutano mkubwa ni kati ya Simba na nyota wao Clatous Chama ambaye inaelezwa kuwa Yanga wamemvutia kasi jambo lililowafanya Simba kupeleka malalamiko Shirikisho la Soka la Mpira Tanzania (TFF).

Habari zinaeleza kuwa mpango wa Yanga upo palepale kumpata nyota huyo iwapo mambo yatakuwa sawa na wataongeza mwingine ambaye ni kipenzi cha wana Simba.

"Katika suala la usajili kwa Bongo kuna siasa nyingi ila hili la Chama liache kuna mwingine anachukuliwa mzimamzima na anatua Jangwani hivyo ni jambo la kusubiri na kuona ni kati ya Kanda ama Chama hapo pana jambo," ilieleza taarifa hiyo.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema kuwa mpango mkubwa kwa sasa upo kwenye kusuka kikosi kipya ambacho kitaleta ushindani msimu ujao.

8 COMMENTS:

  1. Wewe mwandishi uchwara unsjionyesha kabisa lengo lako umetumwa kujaribu kuisumbua simba kisakolojia ila hutafanikiwa. Kama umeemua kuwa mwandishi wa habari punguza mahaba

    ReplyDelete
  2. Duh naona mmeishiwa habari, mnazidi kuua blog yenu mkiendelea hivi.

    ReplyDelete
  3. Enter your comment...Huo ni utopolo mtupu

    ReplyDelete
  4. Hii kumbe ni blog ya yanga kwa jina la soka kiganjani.

    ReplyDelete
  5. Acheni mambo yasiokuwa na msingi wowote tayari mumeambiwa kuwa Chama anamkataba wa mwaka moja uliosalia.Sasa mnataka nini nyie utoporo

    ReplyDelete
  6. Hakuna mchezaji mwenye akili timamu anayeweza kutoka Simba kwenda Utopolo kwa sasa. Labda kama Simba hawamtaki.

    ReplyDelete
  7. Mwandishi hebu punguza ulimbukeni wako.Simba inajua wazi Kanda ni mchezaji wa TP Mazembe na yuko Simba kwa mkopo.Mnahangaika na Simba badala ya kuhangaika na TP Mazembe.Mwandishi kuwa na uweledi wa kutupasha habari vinginevyo ni bora ukashinda Jangwani na kucheza bao, karata na zumna huku mkiendelea kuota ndoto zenu za alinacha.

    ReplyDelete
  8. Labda story ya chama iliuza gazeti kwa hivyo mnajaribu kuzua story nyengine feki.Hii njaa ya corona isiwe sababu ya kukiuka maadili ya uandishi kwani hata mwandishi au gazeti laweza kushtakiwa kwa kusambaza uongo. Kwanza yanga wanatakiwa kumng'ang'anua mwakalibela kabla ya kukumbana na rungu la FIFA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic