UONGOZI wa Yanga
umesema kuwa unawafuatilia wachezaji wote wanaoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara
pamoja na wale wanaoshiriki Ligi Daraja la Kwanza ikiwa ni pamoja na Gwambina
FC ili wapate wachezaji bora watakaomwaga wino msimu ujao.
Habari zinaeleza kuwa
miongoni mwa nyota wanayemtazama ni nahodha wa Gwambina FC, Jacob Massawe
ambaye aliwatungua msimu wa 2018/19 walipokutana Januari 19 wakati akikipiga Stand United.
“Yanga inahitaji kupata
mshambuliaji na kwa sasa inafuatilia kila mchezaji makini ili kuipata saini
yake,miongoni mwa nyota anayetazamwa ni nahodha wa Gwambina, Jacob Massawe
ambaye anaurafiki mkubwa na nyavu na aliwahi kuwafunga pia msimu uliopita,”
ilieleza taarifa hiyo.
Ofisa Habari wa Yanga,
Hassan Bumbuli alisema kuwa wamekuwa wakiwafuatilia wachezaji wote wanaocheza
mpira ikiwa ni pamoja na Gwambina ila kuhusu masuala ya usajili wakati wake
bado.
Massawe ambaye ni
nahodha wa Gwambina msimu huu akiwa na Gwambina inayoshiriki Ligi Daraja la
Kwanza amecheza mechi 17 na kutupia mabao 10.
0 COMMENTS:
Post a Comment