May 7, 2020

KIUNGO wa Polisi Tanzania, anayewindwa na Simba, Yanga na Azam FC huenda akasepa zake na kuibukia Morocco kukipiga soka la kulipwa.

Baraka Majogoro ambaye msimu huu amekuwa kwenye ubora wake inaelezwa kuwa amekuwa akizichonganisha Simba na Yanga ambazo zote zinahaha kuipata saini yake.

Habari zinaeleza kuwa kuna timu moja ambayo ipo Morocco imeshaingia kwenye 18 ikisaka saini yake.

"Tayari Majogoro ameanza mazungumzo na Klabu ya Youssofia Berrechid ya huko Morocco hivyo mambo yakijibu anaweza kusepa," ilieleza taarifa hiyo.

Majogoro amesema kuwa anatazama nafasi yake ya kucheza kwanza kisha dili lenyewe litasema nini.

3 COMMENTS:

  1. Udalali mwingine bhana!!! style unayotumia kuwadalalia wachezaji haina mvuto hata kidogo.Sometime mtu unabaki kucheka tu

    ReplyDelete
  2. Udalali umezidi uwezo.Kila siku kuna jipya na yote hayana msingi.

    ReplyDelete
  3. Ni vyema kuweka wazi watu wajue ni meneja wa mchezaji au wakala kuliko hivi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic