May 22, 2020


OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, ameushauri uongozi wa Klabu ya Yanga kujiandaa vizuri kama ni kweli wanataka kuingia katika mabadiliko ya mfumo wa kiuendeshaji wa klabu yao.

Hivi karibuni, Yanga walikuja na kampeni iliyopewa jina ‘Twenzetu Kwenye Mabadiliko’ wakiwa na dhamira ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo unaosimamiwa na mdhamini wao, Kampuni ya GSM.

Akizungumzia hatua hiyo, Manara alisema: “Kwanza napenda kuwapongeza kwa hatua ambayo wanataka kuiendea.

“Lakini pia napenda kuwakaribisha huku tulipo kwa kuwa Simba tayari ilishapita hatua hiyo na yote kwa yote napenda kuwaasa watani zangu Yanga wajiandae vya kutosha kwani mchakato huu siyo rahisi na unahitaji weledi wa kutosha ikiwemo kubadilisha mtazamo wa kifikra.

3 COMMENTS:

  1. Acha mdomo manara,zungumzia Simba tu,ni vyema ukatuacha na Yanga yetu coz Simba hamna cha kuishauri Yanga wakati nyinyi wenyewe mpaka sasa hakuna mabadiliko yeyote mliyofanya ya kiuendeshaji,Simba bado mpo kwenye mfumo uleule wa zamani wa kumtegemea mzamini,hadi sasa Simba inamtegemea mo km mfazili na si muekezaji..wakati wowote anaweza akawatupa na mkarudi kuombaomba km mwanzo..Hivyo manara kaa kimyaa,usipende kuropoka ropoka..ndio mana umekimbiwa na mke kwa mdomo wako..kudadadeki.

    ReplyDelete
  2. Manara hana akili kwani simba imebadilika nn wakati inaendeshwa kwa mfumo wa ufadhili.Aachane na yanga azungumzie timu yake

    ReplyDelete
  3. Nyie mikia hamuelewi rudun shule.ni sawa na manyumbu tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic