LAMINE Moro, beki wa Yanga amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya shilingi laki tano (500,000/-) kwa kosa la kumkanyaga mchezaji wa JKT Tanzania, Mwinyi Kazimoto.
Kazimoto pia amefungiwa mechi mbili kwa kosa la kusababisha vurugu kwenye mchezo wao uliopigwa Juni 17, 2020 kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mchezo huo JKT Tanzania ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Yanga na kugawana pointi mojamoja.
Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi imeeleza kuwa, Kamati ya Saa 72 pia imepokea malalamiko ya Azam FC kuhusu uamuzi uliofanywa katika mchezo wao dhidi ya Yanga, malalamiko ambayo yamepelekwa kwenye Kamati maamuzi.
Mchezo huo wa Yanga na Azam FC ulikamilika kwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Uhuru.
Azam FC wamepeleka malalamiko yao wakidai kuwa walipaswa kupewa mabao mawili na penalti moja baada ya mchezaji wao kuangushwa ndani ya eneo la penalti.
0 COMMENTS:
Post a Comment