June 25, 2020

YANGA jana ilisubiri mpaka dakika za jioni kabisa kuweka usawa wa kufungana mabao 2-2 na Namungo FC  kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Namungo FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery ilianza kuandika bao la kwanza dakika ya 52 kwa kichwa na bao la pili alilifunga tena dakika ya 70 kwa shuti kali lililomshinda Metacha Mnata.

Yanga ilizunduka kupitia kwa mtupiaji wao namba moja, David Molinga ambaye aliingia dakika ya 57 akitokea benchi.

Alianza kupachika mabao hayo dakika ya 80 na 90 na kuifanya Yanga igawane pointi moja na Namungo.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga ibaki nafasi ya tatu ikiwa na pointi 57 huku Namungo ikiwa na pointi 55 nafasi ya nne zote zimecheza mechi 31.

Mechi ya kwanza waliyocheza Uwanja wa Majaliwa, Machi 15 timu zote zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 hivyo ndani ya dakika 180 zote zimejikusanyia pointi mbili ndani ya msimu wa 2019/20.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic