ANTHONY Martial, nyota wa Manchester United jana alisepa na mpira wake baada ya kutupia mabao matatu mbele ya Sheffield United.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Old Trafford ulikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhaha kusaka pointi tatu.
Mabao hayo yalipachikwa dakika ya 7, 44 na 74 na kuwafanya wasepe na pointi zote tatu.
Ushindi huo unaifanya United kufikisha pointi 49 kibindoni ikiwa nafasi ya tano huku Sheffield ikiwa na pointi 44 nafasi ya nane zote zimecheza mechi 31.
Mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Norwich City, Juni 27, inahaha kupata ushindi ili kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
0 COMMENTS:
Post a Comment