IHEFU FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza hesabu zake kubwa kwa sasa ni kuona inashinda mechi mbili zilizobaki ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2020/21.
Ikiwa kundi A ina pambana vikali na vinara wa kundi hilo ambao ni Dodoma FC iliyo nafasi ya kwanza kwa kuwazidi mabao matano kibindoni.
Timu zote mbili zimecheza mechi 20 na kibindoni zina pointi 45. Ihefu imefunga mabao 28 huku Dodoma ikiwa imefunga mabao 33 kibindoni.
Mechi zake mbili ni dhidi ya Friends Rangers Julai 4 na Cosmopolitan FC, Julai 11 zote zinachezwa Uwanja wa Highland Estates, Mbarali, Mbeya.
Nyota wao Lulanga Mapunda amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya ushindani na hesabu zao ni kuona wanashinda mechi zote ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki ligi kuu.
"Tuna kazi ngumu na kubwa, ushindani ni mkubwa ila tutapambana kupata matokeo chanya kwa mechi zetu mbili ambazo zimebaki, kikubwa mashabiki wazidi kutupa sapoti," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment