HASSAN Kabunda, winga wa KMC leo alimaliza msumari wake wa mwisho kwa kumtungua mlinda mlango wa Yanga bao la kideo kwa mpira wa adhabu uliomshinda Metacha Mnata wakati Yanga ikikubali kulala kwa mabao 3-0.
Mchezo wa leo wa kirafiki ulichezwa ulichezwa Uwanja wa Uhuru ambapo ushindani ulikuwa mkubwa kwa timu zote mbili.
KMC ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Sadala Lipangile dakika ya 31 kwa pasi ya Charlse Ilanfya na bao la pili likapachikwa na Ilanfya kwa pasi ya Emmanuel Mvuyekule.
Mchezo unaofuata wa Yanga utakuwa dhidi ya Mwadui ambao utakuwa ni wa Ligi Kuu Bara inayoendelea mzunguko wa pili.
Mmmmmmm
ReplyDeleteHakuna timu hapo timu yenu ipo kwenye magazeti ya champion na hilo lingine na hii blog ya salehe jembe ya kusifiwa kutwa ndio hiyo ilipigwa 3 na watoto wadogo mara tumesajiri nani mara hivi GONGOWAZI aibu yaooooo
ReplyDeleteNa kesho muweke ukurasa wa mbele tatu hizo tuone GONGOWAZI na gazeti lenu la champion
ReplyDeleteKwa kweli watani walikuwa taabani Sana kama vile wanyonge, Hawana hamu wapole walioishiwa na nguvu na kama waliolazimishwa. Yuko wapi Nguaz, kalala mapema
ReplyDeleteTatizo hili limeletwa na gazeti la Champion.Kazi imekuwa ni kuwasifia Yanga kwenye kila kitu bila kuwaeleza udhaifu wetu.Huwezi kuwa na timu ipo pointi 20 nyuma ya mpinzani wetu halafu baada ya kutafuta suluhisho tunaridhika na sifa za kijinga za gazeti la Champion.
ReplyDeleteMkwasa sio Kocha. Kama Luc atachelewa afadhali timu apewe Said Maulid. Vinginevyo hatutoki kwa Kagera. Timu hata Paso tatu haipigi, kila Mpira ni kubutua mbele tu.
ReplyDeleteEnter your comment...poleni utopolo fc kwa staili hii mtaugua vidonda vya tumbo bure
ReplyDelete"Kwa Yanga hii jiandaeni" hata hiyo Jana wanaendelea kujinasibu. Hesabu yao ipo hivi, watashinda michezo yao iliyobakia na huku Mnyama atashindwa michezo yote iliyobakia. Hii ni kunyanyua morali ya GSM.
ReplyDeleteMadhaifu mengi yamejionyesha niliyajua haya yatatokea baada ya kusikia benchi halijakamilika makocha watatu muhimu kuleta fitness ya wachezaji hawapo..vile vile niliposikia timu haijaingia kambini pia niliposikia wachezaji wameongezeka uzito niliposikia mkurugenzi wa mashindano wa Yanga Anaitwa Thabiti Kandoro (Simba Damu) na kutokuwepo kwa mkurugenzi wa ufundi niliposikia nahodha ni majeruhi nilijua kuna siku majibu yake ya kupoteza mechi yatakuja...kwakweli kama hii ndiyo Yanga wenyewe hii....kweli Twenzetu kwenye Mabadiliko kwani 65% ya wachezaji wa Yanga hawastahili kuivaa jezi ya njano na kijani ya klabu hai kongwe kabisa, mabadiliko yaguse Sekretariati na baadhi ya benchi la ufundi....Twenzetu Kwenye Mabadiliko
ReplyDeletePoleni kama nyinyi mnaona ushindani ni wa Simba!!! KMC anawatungua kwa mara ya pili, awali ilikuwa bahati na leo bao tatu (3) sijui nayo ni bahati au mchezo uliwazidi.
ReplyDelete