BEKI wa zamani wa Machester United, Phil Neville amesema kuwa Manchester United inahitaji kuongeza beki mwingine ambaye ataongeza ulinzi kwenye kikosi hicho ambaye atakuwa na matokeo ndani ya timu mithili ya Virgil Van Dijk wa Liverpool.
Ole Gunnar Solskajer, Kocha Mkuu wa Manchester United alilazimika kushinda jana kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali ya Kombe la FA muda wa nyongeza mbele ya Norwich kwa bao lililofungwa na Harry Maguire ambaye dau lake la usajili lilikuwa ni pauni milioni 80.
Safu ya United ilishindwa kulilinda bao lililopachikwa dakika ya 51 na Odion Ighalo ambalo lilisawazishwa na nyota wa Norwich, Todd Cantwell dakika ya 75 kabla ya lile la ushindi kufungwa na Maguire dakika ya 118 kwenye muda wa nyongeza.
Kwenye mchezo huo, Timm Klose wa Norwich alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 88 na kuwafanya wamalize wakiwa pungufu kutokana na adhabu hiyo.
Phil amesema:"Nafikiri timu inahitaji kupata zaidi ya nyota mwingine kwenye upande wa mabeki, iwe mfano wa Dijk namna ambavyo amekuwa egemeo ndani ya Liverpool ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England."
0 COMMENTS:
Post a Comment