INAELEZWA kuwa sababu kubwa ya Yanga kukaa kikao kizito na Bernard Morrison, kwa zaidi ya saa tatu ni kukweka mambo sawa kutokana na suala lake la mkataba kuleta mkanganyiko.
Morrison alitua Yanga katika dirisha dogo la usajili msimu huu, ambapo hadi sasa amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao manne na pasi tatu kwenye mashindano yote ya jumla.
Morrison anasema mkataba wake unamalizika baada ya ligi kuisha huku Yanga wakidai walimuongeza miaka miwili hivyo unamalizika Julai, 2022.
Kitendo hiki kimeufanya kila upande uzungumze kwenye vyombo mbalimbali vya habari huku Morrison akitumia Gazeti la Championi kama sehemu sahihi ya yeye kufikisha ujumbe kwa kuwa anajua linafika sehemu kubwa Tanzania, jamaa alitiririka kwelikweli, pia unaweza kumcheki live kupitia Global TV Online.
Habari kutoka ndani ya Yanga, zimeweka wazi kuwa,hivi karibuni uongozi wa timu hiyo ulikutana na Morrison kwenye kambi yao iliyopo Regency Hotel, Mikocheni jijini Dar na kumuweka chini kwa zaidi ya saa tatu ikimtaka aweke wazi madai yake ya kusema hajasaini miaka miwili ndani klabu hiyo.
“Morrison ameendelea kuonyesha jeuri kubwa sana kwetu, jambo ambalo sasa tumeamua nasi kumuonyesha kuwa hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya klabu yetu, hivyo tuliamua kumuita na kukaa naye ili aseme nia yake nini hadi aamue kutangaza hana mkataba wakati anajua aliongeza miaka miwili.
“Suala hili ni kubwa sana kwetu na tunaamini kama Morrison asipobadilika basi ajuwe hao wanaomtuma ili atuvuruge wataishia kumuona tu akiishia benchi maana hatuna jinsi nyingine ya kuendelea kubishana na mtu anayetaka kuipanda kichwani klabu yetu ingawa tunafahamu pia kweli kuna watu wanamshawishi avunje mkataba kinyemela,” kilisema chanzo hicho.
Championi lilimtafuta Morrison ili aweze kuzungumzia ishu ya kikao chake na mabosi wake lakini simu yake iliita na haikupokelewa.
Mmmm Mlimsifia sana hata wachezaji wengine mkawaona hawana maana yoyote.Hivi ninyi utopolo mna shida gani hata mtu akiibukia vichakani akasema yeye ni injinia basi wooote mnaona ni msomi jitathmini sana na hao viongozi wenu isijekuwa darasa mmm
ReplyDeleteTuambie na wewe elimu yako ni ya upeo gani ili tuweze kupima mizani ya maoni yako
DeleteHili suala lina utata mwingi sana. Lakini pia yanga waangalie historia ya huyu jamaa anaweza kuwa mzoefu ktk kutibua mambo
ReplyDelete