June 21, 2020




MTAMBO wa mabao ndani ya Kabu ya Mbao FC iliyo chini ya Kocha Mkuu, Felix Minziro, WAZIR Jr amesema kuwa iwapo masuala ya michezo yatamzingua ataibuka kupiga dili za masuala ya teknolojis ili kupiga mkwanja.

Jr ametupia mabao saba na kutengeneza asi mbili za mabao kati ya 19 ambayo yamefungwa na Mbao FC iliyo nafasi ya 19 na pointi 23.

Akizungumza na Spoti Xtra, Jr alisema kuwa mbali na kucheza mpira ana ujuzi wa masuala ya IT jambo ambalo anaamini kuwa akibuma kwenye soka atapiga hela upande huo.

“Ukiachana na soka mimi nina ujuzi wa masuala ya IT hivyo ninadhani iwapo nitashindwa kuendelea kuwa kwenye masuala ya mpira basi nitapiga madili ya teknolijia kwani huko ndiko ulimwengu ulipo.

“Ninachojua mimi ninaweza kufanya vyote kwa ukamilifu ila kwa sasa nguvu kubwa nimewekeza kwenye masuala ya mpira wakati ukifika nitafanya kazi niliyosomea darasani,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic