June 10, 2020


RAIS wa Kampuni ya La Liga ya Hispania, Javier Tebas ameeleza jinsi La Liga inavyoutazama ushirikiano huo kwa manufaa makubwa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Tebas amesema Mkataba huo na Mabingwa wa Kihistoria na Kampuni ya GSM kama wadhamini ni mwanzo mzuri kwa La Liga kuonyesha uwezo wale katika kubadili na kuleta changamoto mpya ya maendeleo kwenye soka la Afrika.

"Kupiga chapuo uendeshaji wa kiweledi kwa soka la Afrika na Duniani kote ni dhima tulizonazo kama La Liga katika mkakati wa kujitanua kimataifa. Mkataba huu tuliosaini na GSM na Yanga ni mwanzo mzuri kwetu,” amesema Rais huyo wa LaLiga.

"Tunajivunia sana kuhusika katika maendeleo ya klabu ya Yanga kwa sababu huduma hii ya ushauri tunayokwenda kuipa Yanga inakwenda kuwa ya manufaa makubwa," amesema.

5 COMMENTS:

  1. Inaonesha imemtia moyo kuiona mechi Juzi baina KMC na hiyo timu yake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mmmh!! Kweli we ni mkia maana hata kilichozungumzwa na ulichowaza wewe ni tofaut. Ondoa hicho kibanzi

      Delete
    2. Umejipambanua ni jinsi gani kichwa chako kisivyotofautiana na box tupu.

      Delete
    3. hao ndo aina ya mashabiki maandazi wa simba

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic