June 23, 2020




SINGIDA United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ramadhan Nzwanzurimo imezidi kuwa kwenye hali tete baada ya Juni 20 kukubali kichapo cha mbele ya JKT Tanzania huku ikitajwa sababu ni mapumziko ya lazima yaliyosababishwa na janga la Virusi vya Corona.
JKT Tanzania iliinyoosha kwa mabao 2-0 Singida United mabao yaliyofungwa na  Musa Said dakika ya 11 na Hafidh Mussa dakika ya 61.
Matokeo hayo yanafanya Singida United kujichimbia nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 30 ikiwa kwenye hatari ya kushuka daraja.
Ofisa Habari wa Singida United, Calse Katemana amesema kuwa mapumziko ya Corona yaliwafanya washindwe kufanya vizuri ila wana imani ya kurejea kwenye ubora.
“Tulianza kuwa kwenye ubora maana kabla ya Corona tuliwafunga Mbeya City hicho ndicho ambacho tunakitaka ila kwa sasa tunaanza kujipanga upya maana Corona ilituvuruga,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic