June 23, 2020


MEDDIE Kagere,mshambuliaji namba moja wa Simba amenyooshwa vilivyo na wajeda wa Ruvu Shooting kwa kumbana kwa muda wa dakika 165 bila kuambulia bao wala kutengeneza nafasi ya bao.
Kwa msimu wa 2019/20 Simba ikiwa imekutana na Ruvu Shooting mara mbili, mchezo wa kwanza, Uwanja wa Uhuru, Novemba 23 Simba ilishinda mabao 3-0,mabao mawili yalifungwa na Miraj Athuman na bao moja lilifungwa Tairone Santos.
Kagere alitumia dakika 75 kwenye mchezo huo alibanwa mbavu na wajeda hao kwa kushindwa kufurukuta kwa kuwafunga bao.Juni 14 Uwanja wa Uhuru, Kagere tena alibanwa mbavu na Ruvu Shooting ambapo ndani ya dakika 90 alishindwa kufunga wakati Simba ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1.
Kagere ni kinara wa utupiaji ana jumla ya mabao 19 na pasi tano za mabao huku Simba ikiwa imefunga jumla ya mabao 67.
Mabao yake 19 aliwatungua hawa hapa:- Mbeya City bao 1, Lipuli bao 1, JKT Tanzania mabao mawili, Mtibwa Sugar bao 1, Kagera Sugar mabao 3, Azam FC mabao mawili, Biashara United mabao mawili, Yanga bao 1, Alliance bao 1, Namungo 1, Singida United mabao manne.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic