RAMADHAN Nswanzurimo, Kocha Mkuu wa Singida United amesema kuwa anaamini kuwa timu yake ikishuka Daraja msimu huu hakuna ambaye atawashangaa kwa kuwa wanapita kwenye mazingira magumu kuanzia kwenye maandalizi na kukosa ushindi uwanjani.
Akizungumza na Spoti Xtra, Nswazurimo alisema kuwa tatizo kubwa lililopo kwa wachezaji wake kwanza ni kushindwa kumalizia nafasi wanazotengeneza, pamoja na kuwa na matatizo kwenye maandalizi.
"Timu ina matatizo ikiwa ni pamoja na wachezaji kushindwa kumalizia nafasi ambazo wanazitengeneza, kwa mfano mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar kulikuwa na nafasi saba za wazi ila tukapata nafasi moja ya bao tukapoteza kwa kufungwa mabao 3-1.
"Mbali na hiyo pia tumekuwa tukipata mazingira magumu kwenye maandalizi yetu hivyo ninadhani watu wa Singida United hawatakuwa na maswali pale timu itakaposhuka Daraja kwani inapitia mazingira magumu," alisema Nzwanzurimo.
Singida United ipo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 31 ndani ya Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment