KOCHA Mkuu wa Tanzania Prisons, Adolf Rishard amesema kuwa wachezaji wake wapo tayari kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa Juni,28.
Prisons ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na JKT Tanzania kwenye mchezo wake uliopita Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Inakutana na Simba ambayo imetoka kuwatungua mabao 2-0 watani zao Mbeya City kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Akizungumza na Saleh Jembe, Rishard amesema hawana presha kubwa na mchezo wao dhidi ya Simba kwa kuwa anawaamini vijana wake katika kutafuta ushindi.
"Ni mchezo mgumu, utaamuliwa na mbinu ngumu, hakuna haja ya kuhofia kwa kuwa kila mchezo una falsafa zake na mbinu zake kikubwa ni utayari na kuona namna gani tutakuwa kwenye mchezo wetu.
"Malengo yetu makubwa kwa pamoja ni kupata matokeo mazuri ambayo yatazidi kutufanya tuwe kwenye nafasi nzuri kwani hakuna anayepanga kufeli hata sisi hatuna mpango wa kufeli.
"Ninawaheshimu wapinzani wangu hilo ni jambo la kwanza ila ninawatambua vema kwani nimewahi kukutana nao na ni timu nzuri ambayo ina mipango mizuri hivyo ninaamini hautakuwa mchezo mwepesi," amesema.
Tanzania Prisons ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi zake kibindoni 42, inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi zake 78 zote zimecheza mechi 31.
Prisons hesabu zake ni kubaki ndani ya 10 bora huku Simba ikihitaji kushinda ili kutangazwa kuwa mabingwa hapo ndipo ugumu wa mchezo unapoanzia.
Itakuwa ni heshima kubwa kwa Prison kuwa wao ndio waliofanikisha ubingwa wa Mnyama kwa mara ya tatu mfululizo
ReplyDelete