June 23, 2020



HARUNA Niyonzima, kiungo mshambuliaji wa Yanga mwenye uwezo wa kucheza na mpira namna anavyotaka amesema kuwa hawaachi kitu kwenye mechi zote watakazocheza ndani ya Ligi Kuu Bara.
Yanga imecheza jumla ya mechi 30 kibindoni ina pointi zake 56 imebakiza mechi nane ili kukamilisha mzunguko wa pili.
Akizungumza na Saleh Jembe, Niyonzima amesema kuwa wachezaji kwa pamoja wamekubaliana kuendelea kushirikiana ili kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
“Tuna mechi ngumu kwenye ligi hilo lipo wazi kwani kwa sasa timu nyingi zinapambana hasa ukizingatia ni lala salama, nasi tuna mipango yetu ya kutoacha kushinda kwenye mechi ambazo tutacheza.
“Kitu cha msingi ni kuona tunakusanya pointi tatu ambazo zitatufanya tuzidi kuwa kwenye nafasi nzuri, hatutaki kumaliza tukiwa nafasi ya tatu tunahitaji ya pili,” amesema Niyonzima.
 Kesho, Juni 24, Yanga itamenyana na Namungo, Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni.

7 COMMENTS:

  1. Haha Yanga Hatuwachi kitu. Words are too cheap, but action is too hard na huku porojo likiendelea na ushindi kwa kila mechi

    ReplyDelete
  2. Ujinga umewajaa na ukanjanja,kazi kubebwa tu ndicho mnachokitegemea hamna lolote.

    ReplyDelete
  3. Ndio walivo mabingwa wa jadi. Hawa kila wanapochapwa huangusha kilio cha kuonewa au utawasikia wakilalama kwa makundi "jamani sisi tunaumia Kipre hatumtaki hata kumuona huko mitaani hatuna pakukaa na Kocha hafai" wakati Mnyama akishindwa au kupata Droo haya huyasikii kabisa hawajui kuwa haya yanamuumiza mfadhili anayejitolea kwa mamilion na wanapchapwa husingizia ubaya wa viwanja au kuwa wanachoka kusafiri kwa mabasi kama vile hayo ya pekeyao

    ReplyDelete
  4. Hebu chezeni mpira acheni maneno Yanga. Tunataka kabumbu siyo maneno.

    ReplyDelete
  5. Hata hiyo pointi moja waliyoipata Kutoka Azam hawakustahiki kukipata na Azam imeshapeleka mashtaka huko TFF kutokana na magoli mawili ya wazi waliyonyimwa na penelti iliyokataliwa pamoja na ushahidi kamili ya hayo

    ReplyDelete
  6. Bora Yanga wanatumia nguvu zao kuliko nyie Simba kazi yenu sasa hivi ni kununua mechi tu. Uwezo wenu halisi ni ule mlilocheza Ruvu Shooting ya Masau Bwire

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic