July 29, 2020


INAELEZWA kuwa baada ya Yanga kuachana na Luc Eymael ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo wanapiga hesabu za kuwavutia kasi makocha wenye uzoefu na Ligi Kuu Bara ambao ni Patrick Aussems na Hitimana Thiery.

Habari zinaeleza kuwa kuna majina zaidi ya 18 ambayo yametua mezani kwa Yanga kuomba kazi ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa kihistoria.

"Tayari Yanga imeanza mchakato wa kumleta kocha mpya ambaye atafanya kazi ya kukinoa kikosi kwa ajili ya msimu ujao na miongoni mwa wale ambao wanahitajika ni pamoja na Aussems na Thiery wa Namungo.

"Thiery amekuwa bora kwani amemaliza ligi akiwa ndani ya tano bora na aliweza kuwasumbua Yanga hata Simba walipokutana ndani ya uwanja, hivyo anaweza kutua pale, Aussems pia anatajwa kuingia kwenye dili hilo kwani ana uwezo mkubwa na anaitambua Yanga na ligi ya Bongo" ilieleza taarifa hiyo.

Thiery amesema kuwa kwa sasa yupo na Namungo hivyo msimu ukiisha atajua mambo yatakuaje. 

Kaimu Katibu wa Yanga, Simon Patrick amesema kuwa kwa sasa wanaendelea na mchakato wa kumtafuta kocha mambo yakiwa sawa wataweka kila kitu wazi.

2 COMMENTS:

  1. Aussemms watamuwezs maana Simba walimpa huduma zote anazostahili wao hata DStv wameshindwa kumuwekea

    ReplyDelete
  2. Aussems ni kocha mzuri na atawafaa sana Yanga. Kikubwa huyo GSM ajiandae gharama zake maana huyo ni mzee wa bata kweli kweli na hataki kupangiwa nyumba yeye atakaa hoteli ya nyota 5 maisha yake yote atakayokuwa Yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic