July 14, 2020

BIASHARA United iliyo chini ya Kocha Mkuu,  Francis Baraza leo ina kazi ya kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa majira ya saa 10:00.

Baraza ameweka rekodi ya kucheza mechi 10 bila kuyeyusha pointi tatu kwenye uwanja Uwanja wa nyumbani ambapo mechi zake tatu aligawana pointi tatu na timu zilizotua hapo kwa kulazimisha sare.

Hivi karibuni  alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Azam FC ikafuata sare ya bila kufungana na Yanga kisha  alipata sare ya bila kufungana na Ruvu Shooting. 

Baraza amesema kuwa malengo makubwa ya timu ni kumaliza ikiwa ndani ya 10 bora ili wapate hali ya kujiamini zaidi msimu ujao.

"Kwa sasa naweza kusema ligi safari yake ndo imemalizika hasa baada ya bingwa kupatikana lakini sio mwisho wa mapambano hasa katika kufikia malengo yetu ya kuwa ndani ya 10 bora bado tuna kazi ya kufanya," amesema.

Biashara United ipo nafasi ya tisa ikiwa na pointi 46 inakutana na Polisi Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu,  Malale Hamsini ikiwa na pointi 48 nafasi ya sita zote zimecheza mechi 34.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic