July 20, 2020


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema hatakuwa na huduma ya wachezaji wake wawili, Haruna Niyonzima na Mapinduzi Balama ndani ya Yanga mpaka msimu ujao wa 2020/21.

Viungo hao kwa pamoja wamehusika kwenye jumla ya mabao matano ndani ya Yanga katika ligi kuu, Niyonzima akiwa amefunga bao moja, huku Mapinduzi akitupia matatu na asisti moja.

Eymael amesema kuwa viungo hao wanasumbuliwa na majeraha ambayo yatawafanya wakae nje ya uwanja hadi msimu huu unamalizika.

“Niyonzima na Mapinduzi sitakuwa nao kwenye mechi za ushindani zilizobaki kwa sasa mpaka msimu ujao kwa kuwa wanasumbuliwa na majeraha, hivyo ninaamini watakapokuwa fiti watarejea uwanjani kwa ajili ya msimu ujao,” amesema Eymael.

Niyonzima anasumbuliwa na maumivu ya goti, aliyapata kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United, lakini baadaye akacheza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Simba ambapo inaelezwa alisikia maumivu, akatolewa, huku Mapinduzi akiumia kwenye mazoezi wakati Yanga ilipokuwa inajiandaa kucheza na Ndanda.

Kwa sasa, Yanga inajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Julai 22, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

2 COMMENTS:

  1. Niyo ni mchezaji mkubwa na mzoefu, alikubalije kuendelea kuiuiza kwa kulikuza jeraha lake kisa ni mechi ya Simba? Kweli kocha wa Yanga aliishiwa mbinu na mchezaji mwingine zaidi ya Niyo? Mungu amnusuru tu jeraha lisije likawa kikwazo hata tukashindwa kumwona msimu ujao, ana familia inayomtegemea huyo akiwemo binti wa Kitanzania.

    ReplyDelete
  2. Kwanini basi yeye alisema karudi Yanga kuipa ubingwa. Namsihi asubiri mpaka atapotimiza ahadi yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic