July 20, 2020


MTUPIAJI namba moja kwa wazawa ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Yusuph Mhilu amesema kuwa isingekuwa majeruha angefunga mabao mengi na kuleta ushindani kwa mtupiaji namba moja, Meddie Kagere.

Mhilu ametupia jumla ya mabao 13 akiachwa kwa mbali na Kagere raia wa Rwanda  mwenye mabao 22 akiwa ni namba moja kwa sasa kwa utupiaji. 

Akizungumza na Saleh Jembe, Mhilu amesema kuwa amekuwa akishindwa kuendeleza moto wake ndani ya uwanja kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara.

"Namshukuru Mungu nimekuwa nikipata nafasi ya kucheza na kufunga ninafunga ila nina amini isingekuwa kusumbuliwa na majeruhi ningekuwa nimefunga mabao mengi kwa ajili ya kutimiza wajibu wangu ndani ya timu.

"Ila kwa kuwa nimekuwa nasumbuliwa na majeruhi imekuwa ikinipa wakati mgumu kufikia malengo ambayo nimejiwekea ila nina amini bado uwezo ninao," amesema.

Mhilu kwa sasa anatibu majeraha ya nyama za paja aliyopata hivi karibuni kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo huo ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 kwa sasa amesema anaendelea vizuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic