BEKI wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’, amesema kuwa yupo fiti kwa asilimia zote, lakini anashangaa kwa nini hachezi ndani ya kikosi hicho.
Dante awali alitajwa kujiondoa Yanga kwa madai ya kushinikiza malipo ya fedha zake za usajili, lakini alirejea kikosini baada ya jambo lake kuwekwa sawa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Dante amesema amekuwa akijitahidi kuonyesha uwezo wake na kujituma mazoezini, lakini hapati nafasi.
“Tangu nimerejea kwenye kikosi nimekuwa nikijituma kufanya mazoezi ya pamoja na wenzangu, hivyo naamini kwa kiasi kikubwa niko fiti kwa ajili ya kupambana kwenye mchezo wowote.
“Lakini kwa bahati mbaya nimekuwa sipati nafasi ya kutosha na kiukweli kama utaniuliza ni kwa nini hali hiyo inatokea basi nitakujibu sijui,” alisema Dante.
Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa imecheza jumla ya mechi 35 na kibindoni ina pointi 67.
Leo ina kibarua cha kumenyana na Mwadui FC kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 1:00 usiku, Uwanja wa Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment