July 18, 2020


THOBIAS Kifaru,  Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kuwa leo watashinda mchezo wao wa Ligi Kuu Bara mbele ya KMC utakaopigwa Uwanja wa Gairo, Morogoro.

Mtibwa Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuberi Katwila imetoka kushinda mchezo wake uliopita mbele ya Azam FC kwa kupata bao 1-0 inakutana na KMC ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0 mbele ya Lipuli FC Uwanja wa Samora.

Timu zote mbili zinapambana kusaka nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na kutokuwa na uhakika wa kubaki msimu ujao iwapo watapoteza mechi zao tatu zilizobaki.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 41, KMC ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 43 zote zimecheza mechi 35.

Kifaru amesema:"Mchezo wetu uliopita tulishinda mbele ya Azam FC na tutashinda pia mbele ya KMC," .

Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic